DIWANI hii ya N‘na Kwetu: Sauti ya Mgeni Ugenini ilishinda kwenye awamu ya kwanza ya Tuzo za Fasihi ya Afrika kwa Lugha ya Kiswahili inayotolewa na Wakfu wa Mabati-Cornell mwaka 2015. Tungo nyingi zilizomo humu ziliandikwa baina ya robo ya mwisho ya mwaka 2010 na nusu ya mwanzo ya mwaka 2015. Hii ni miaka mitano ya mwanzo ya mshairi kuhamia na kuishi nchini Ujerumani - mbali na nyumbani kwao, Zanzibar. Ndani yake, kwa hivyo, muna muakisiko wa hisia za mgeni ugenini, akitayamani mengi mazuri ya kwao na akijutia kuyaacha nyuma yake. Ukweli ni kuwa wakati mtu anapoishi ugenini, ndipo hasa ile thamani ya kwao anapoitambua na kutaka kujitambulisha nayo zaidi na zaidi. Ndipo hisia za kutambuwa kuwa ana kwao zinapopanda kiwango cha juu. Kutoka kipembe cha mbali, Mohammed Ghassanani anakuangalia kwao na kuyaona mambo ambayo alipokuwamo ndani yake, alikuwa hata hajui kama yapo. Chembilecho Wajapani: "Samaki hajijui kuwa amerowa!" Na sababu ya kutokujijuwa huko, kwa hakika, ni kwa kuwa yeye mwenyewe anaishi ndani ya maji muda wote.
Die bei uns gelisteten Preise basieren auf Angaben der gelisteten Händler zum Zeitpunkt unserer Datenabfrage. Diese erfolgt einmal täglich. Von diesem Zeitpunkt bis jetzt können sich die Preise bei den einzelnen Händlern jedoch geändert haben. Bitte prüfen sie auf der Zielseite die endgültigen Preise.
Die Sortierung auf unserer Seite erfolgt nach dem besten Preis oder nach bester Relevanz für Suchbegriffe (je nach Auswahl).
Für manche Artikel bekommen wir beim Kauf über die verlinkte Seite eine Provision gezahlt. Ob es eine Provision gibt und wie hoch diese ausfällt, hat keinen Einfluß auf die Suchergebnisse oder deren Sortierung.
Unser Preisvergleich listet nicht alle Onlineshops. Möglicherweise gibt es auf anderen bei uns nicht gelisteten Shops günstigere Preise oder eine andere Auswahl an Angeboten.
Versandkosten sind in den angezeigten Preisen und der Sortierung nicht inkludiert.
* - Angaben ohne Gewähr. Preise und Versandkosten können sich zwischenzeitlich geändert haben. Bitte prüfen sie vor dem Kauf auf der jeweiligen Seite, ob die Preise sowie Versandkosten noch aktuell sind.